Connect with us

Makala

Feitoto Akimbilia Cas

Wakala anayemsimamia mchezaji Feisal Salum ajulikanaye kama Salum Nduruma amethibitisha kuwa mchezaji huyo atakata rufaa katika mahakama ya michezo ya kimataifa (Cas) katika suala lake la mgogoro wa kimkataba na klabu yake ya Yanga sc ambapo imeamliwa kuwa mchezaji huyo bado ni mali ya klabu hiyo.

Yanga sc ilifungua shauri katika kamati hiyo ikilalamika kuwa mchezaji huyo amevunja mkataba pasipo kufuata utaratibu na baada ya masikilizano ya pande zote mbili kamati hiyo iliamua kuwa Feisal bado ni mchezaji wa klabu ya Yanga sc kwani amevunja mkataba pasipo kufuata utaratibu.

Kutokana na maamuzi hayo mchezaji huyo ameonyesha nia ya kukata rufaa katika mahakama hiyo akidai kuwa hajaridhika na maamuzi hayo kutoka kwa kamati hiyo huku akisubiri nakala ya hukumu ili aweze kukata rufaa ambapo mpaka tunaingia mitamboni nakala tayari ameshatumiwa na kilichobaki ni kuanza taratibu za kukata rufaa.

“Mpaka sasa hivi Fei msimamo wake ni ule ule kwamba hana mpango wa kurejea Yanga sc na tumeongea nae jana tu amesema anataka kuendelea kupinga hayo maamuzi kwa kuendelea mbele”Alisema wakala huyo wakati akizungumza na Radio Uhai Fm ya jijini Dar es salaam.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala