Sakata la muda mrefu la kiungo Feisal Salum na klabu ya Yanga sc limefikia tamati baada ya klabu ya Azam Fc kuwasilisha ofa na hatimaye kumnunua mchezaji huyo na leo ametambulishwa rasmi kama mchezaji wa Azam Fc.
Awali ilianza kama tetesi za mchezaji huyo kuhitajika na matajiri hao wa chamazi lakin sasa ni rasmi licha ya dili hili kulazimika Rais Samia kuingilia kati na kusisitiza busara zaidi zimtumike ili kumaliza mgogoro huo uliodumu kwa muda wa miezi takribani sita.
Feisal aliondoka klabuni Yanga sc tangu mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka jana akishinikiza kuondoka klabuni hapo baada ya kulipa kiasi cha shilingi milioni 112 kuvunja mkataba wake na Yanga sc hali iliyoilazimu kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kuingilia na kumuamuru mchezaji huyo kurejea Yanga sc ambapo mchezaji huyo aligoma na kuamua kwenda mahakama ya juu ya usuluhishi wa migogoro ya michezo(Cas).
Kutokana na hali hiyo Rais Samia aliwaomba Yanga sc kumaliza mzozo huo wakati timu hiyo ilifika ikulu kwa hafla ya chakula cha jioni siku ya Jumatatu jioni.
Kutokana na kauli hiyo ya Rais Samia iliwalazimu Yanga sc ikutane na Feisal kumaliza suala hilo huku Azam Fc wakiweka ofa mezani na kufanikiwa kumnasa kiungo huyo na leo kumtambulisha huku wakimkabidhi jezi namba sita ambapo amesaini mkataba wa miaka mitatu.