Connect with us

Makala

Feisal Akwama Tena Tff

Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji ya shirikisho la soka nchini Tanzania(TFF) imetupilia mbali rufaa iliyokatwa na mchezaji Feisal Salum katika kesi yake ya kimkataba na klabu ya Yanga sc ambapo klabu hiyo ilimshtaki mchezaji huyo kwa kuvunja mkataba kinyume na utaratibu.

Katika kesi ya awali iliamliwa na mamlaka hiyo ya soka kuwa mchezaji huyo hajafuata utaratibu katika kuvunja mkataba huo na hivy bado ni mchezji halali wa klabu hiyo ambapo mchezaji huyo aliamua kukata rufaa katika kamati hiyo akiomba marejeo kwa kuitaka kamati ipitie upya shauri hilo ambapo majibu ni kuwa bado mchezaji huyo ni mchezaji halali wa klabu ya Yanga sc.

Kutokana na maamuzi hayo wakili wa mchezaji huyo Fatma Karume amesema kwamba wanasubiri kutumiwa nakala ya hukumu kisha ndio watajua kama wanakata rufaa ama vipi.

“Alichokifanya Feisal na Watu wake ni kuleta mambo ya Kiswahili ambayo hayawezi kumsaidia, Mimi naamini Yanga sio kwamba wanataka kumkomoa, baada ya majibu ya shauri kutoka nilfuatilia Je, hapa kati kati Mchezaji alijaribu kuonana na Yanga ? Hajawahi kwenda lakini huko nje anadai haki yake.”

“Kama washauri wakimwambia Feisal aende wakae mezani , saa 24 ni nyingi jambo litapatiwa ufumbuzi na maisha yataendelea , lakini akitaka kutunishiana hivi anayeathirika ni Mchezaji”Alisema mchambuzi wa masuala ya soka nchini Shaffih Dauda

Awali mwishoni mwa mwaka jana mchezaji huyo aliwasilisha barua ya kuvunja mkataba katika klabu hiyo huku akilipa kiasi cha shilingi milioni 112 kama fidia ya mkataba na hapo ndipo mgogoro na klabu ya Yanga sc ulipoanza ambapo klabu hiyo ilimshtaki Tff.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala