Connect with us

Makala

Fei Toto Kuikosa Azam Fc

Kiungo wa klabu ya Yanga sc Feisal Salum ataukosa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc baada ya kuumia msuli ambao utamfanya akae nje ya uwanja kwa wiki mbili ili kupona tatizo hilo.

Awali inaelezwa kwamba Feisal mwenye mabao manne katika ligi kuu aliumia tangu January 26 ambapo alipatiwa matibabu na kupona hivyo majeraha hayo ni ya kujitonesha katika jeraha la mwanzo wakati akiwa katika mazoezi ya timu ya taifa baada ya mchezo dhidi ya Afrika ya kati.

Baada ya kupata majeraha hayo alifanyiwa vipimo vya kina na kubainika tatizo lake litamweka nje ya uwanja kwa muda usiopungua wiki mbili na alipewa ruhusa ya kutoka kambini kwenda nyumbani kwao Zanzibar.

“Nitakuwa nje ya uwanja kwa muda usiopungua wiki mbili baada ya kupata maumivu ya goti, nipo nyumbani Zanzibar naendelea na matibabu, naamini baada ya muda huo nitakuwa sawa,” alisema Fei aliyeifungia Yanga mabao manne hadi sasa kwenye Ligi Kuu Bara” Alisema Feisal

Yanga sc inatarajiwa kuwavaa Azam fc katika mchezo wa ligi kuu utakaofanyika April 6 katika uwanja wa Azam Complex jijini Dar es salaam mchezo ambao utaamua hatma ya Yanga sc kuelekea mbio za ubingwa wa ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala