Connect with us

Makala

Etoo Kujiuzuru Urais Cameroon

Rais wa Shirikisho la soka nchini Cameroon (Fecafoot) Samuel Etoo ameandika barua ya kujiuzuru nafasi yake hiyo kutokana na timu ya Taifa ya nchini kufanya vibaya katika michuano ya mataifa ya Afrika(Afcon 2023) yanayoendelea nchini Ivory Coast.

Cameroon ilitolewa katika michuano hiyo katika hatua ya 16 bora baada ya kufungwa mabao 2-0 na Nigeria katika mchezo ambao viwango vya wachezaji wa Cameroon vilikua chini tangu mchezo wa kwanza tofauti na matarajio ya wengi.

Etoo siku ya Jumatatu katika kikao cha tathmini juu ya muendelezo wa timu ya Taifa ya nchi hiyo kutokana na kiwango duni cha afcon aliwasilisha barua hiyo ya kujiuzuru mbele ya Kamati kuu ya Shirikisho hilo la soka huku akiwaomba na wao wajiuzuru lakini kamati hiyo iligoma kujiuzuru huku ikisema kuwa bado ina imani nae katika kukuza soka la nchi hiyo.

Etoo tangu awe Rais wa Shirikisho la soka nchini humo amekumbana na misukosuko ya kutosha katika kipindi cha miaka miwili na nusu alichokalia kiti hicho huku kutokuelewana kwake na kipa wa klabu ya Manchester United Andre Onana kukisababisha kipa huyo kujiuzuru kuchezea timu ya taifa kabla ya kuamua kurejea kwa mara ya pili.

Etoo amekua mfungaji wa muda wote wa timu ya Taifa ya Cameroon akifunga mabao 56 katika michezo 118 ya nchi hiyo katika muda wote.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala