Connect with us

Makala

Dube Yupo Sana Azam Fc

Mshambuliaji wa klabu ya Azam FC Prince Dube amesaini mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu yake hiyo Kwa miaka miwili zaidi baada ya ule wa awali kuelekea ukingoni mwishoni mwa mwezi huu.

Mchezaji huyo raia wa Zimbabwe amesaini mkataba huo kuendelea kusalia klabuni hapo mitaa ya Chamazi jijini Dar es salaam mpaka mwaka 2025 huku akiwa amekaa klabuni hapo tangu msimu wa 2020/2021 alipojiunga na timu hiyo akitokea Highlanders Fc ya nchini kwao Zimbambwe.

Mshambuliaji huyo bado ni lulu ikizingatiwa ana umri wa miaka 26 tu huku msimu huu akiwa na klabu ya Azam Fc amemaliza msimu na mabao 12 ya ligi kuu ya Nbc nchini huku akiisadia klabu yake kumaliza katika nafasi ya tatu na kufika fainali katika michuano ya kombe la shirikisho la Azam Fc ambapo wamefungwa na Yanga sc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala