Connect with us

Makala

Drogba Kocha Mkuu Ivory Coast

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza Didier Drogba ametangazwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ivory Coast kwa mkataba wa miaka minne akichukua nafasi ya Jean-Louis Gasset aliyedumu katika nafasi hiyo takribani mwaka mmoja pekee.

Hii ni mara ya kwanza kwa mchezaji huyo wa zamani wa taifa hilo kupata wadhifa wa kuwa kocha mkuu baada ya kumaliza mafunzo ya ukocha ambapo ana leseni ya UEFA PRO aliyopata hivi karibuni.

Aidha inaelezwa kuwa Drogba amemuomba Yaya Toure kuungana nae kama kocha msaidizi na anasubiri majibu kutoka kwa mchezaji huyo mwenzake wa zamani.

โ€œNi fahari kwangu kurudi Afrika na kuanza taaluma yangu ya ukochaย  katika nchi yangu,Nimezungumza na Yaya Toure kuja kuungana nami kama msaidizi wangu na ninasubiri jibu lake labda atanikubalia”.

Drogba amepewa vipaumbele vya shirikisho kumpa wadhifa huo ni kushinda kombe la mataifa ya Afrika 2024 na 2025 na kuhakikisha anaiongoza Ivory coast kushinda taji la kombe la dunia 2026.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala