Connect with us

Makala

Dodoma Jiji Kuweka Kambi Arusha

Klabu ya Soka ya Dodoma Jiji Fc imepanga kwenda kuweka kambi maalumu ya mafunzo jijini Arusha ili kujiandaa na michezo ya duru ya pili ya ligi kuu ya Nbc nchini.

Katika Kambi hiyo timu hiyo pamoja na Mafunzo pia  imepanga kucheza michezo miwili ya kirafiki kujiandaa na michezo ya Ligi kuu ambapo itaanza kuzisaka alama tatu mbele ya Pamba Jiji katika uwanja wa Jamhuri Dodoma Februari 05.

Mtendaji Mkuu wa Dodoma Jiji FC, Johnson Fourtnatus alisema kuwa kambi hiyo ni maalumu kuongeza mbinu za kiufundi kwa wachezaji.

“Tumekubaliana kwenda kuweka kambi mkoani Arusha kwa muda wa siku sita, na tutacheza michezo miwili ya kirafiki na timu zinazoshiriki Ligi daraja la kwanza Tanzania bara, tukianzia kesho ambapo tutacheza na Mbuni FC, na tarehe 31 tutacheza mchezo wa mwisho wa kirafiki kukamilisha kambi yetu na tarehe 2 Februari, 2025 timu itarudi Dodoma kuendelea na kambi kuelekea mchezo dhidi ya Pamba Jiji Fc”,Alisema Fortunatus.

Katika hatua nyingine Fortnatus akaweka wazi mpango mkakati wa klabu ya Dodoma Jiji FC, katika duru ya pili ya Ligi kuu Tanzania bara.

“Mpango wetu ni kuhakikisha timu inaendelea kubaki kwenye Ligi kwa msimu huu na pia kuhakikisha tunatoa burudani kwa wapenzi, mashabiki na wana Dodoma kwa ujumla kwa kucheza mpira mzuri na wenye matokeo chanya”,Alisema.

“Katika kufanikisha hilo katika dirisha dogo la usajili tumefanya usajili wa wachezaji wawili ambao ni beki wa kati Abdi Banda na Mukrim Issa ambaye tumemchukua kwa mkopo kutoka Singida Black Stars” alisema Fourtnatus”,Alimalizia kusema

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala