Licha ya taarifa kudai kuwa dili la beki Djuma Shabani kujiunga na klabu ya Azam Fc limeshindikana uhakika ni kwamba mchezaji huyo ameanza mazoezi na kikosi cha timu hiyo huku taarifa mpya zikidai kuwa tayari alishamalizana na klabu hiyo na kinachosubiriwa na kuanza kuitumikia tu.
Djuma ameonekana katika mazoezi ya klabu hiyo huku tayari taarifa zikidai kuwa ameshasaini mkataba wa kujiunga na matajiri hao japo ataanza kutumika mwezi januari baada ya dirisha dogo kutokana na kutopatikana kwa nafasi baada ya idadi ya wachezaji wa kigeni klabuni hapo kuwa imekamilika.
Azam Fc ilikua na mpango wa kumtoa kwa mkopo golikipa Ali Ahmada lakini suala hilo lilishindakana dakika za mwisho za usajili baada ya mchezaji huyo kugoma akihofia hatopata timu nzuri.
Djuma anatarajiwa kuungana na Yannick Bangala pamoja na Feisal Salum ambao wote watatu wameitumikia Yanga sc kwa mafanikio makubwa na kuamua kuachana na klabu hiyo kwa nyakati tofauti tofauti ambapo Bangala na Feisal waliuzwa kwa dau la jumla la Tsh 300 milioni huku Djuma akivunja mkataba kwa makubaliano ya pande mbili.
Azam Fc msimu huu imeanza vibaya michuano ya kimataifa baada ya kutolewa katika hatua za awali za kombe la shirikisho na klabu ya Bahil Kanema ya nchini Ethiopia kwa matuta hivyo inahitaji kuboresha baadhi ya maeneo ya msingi ili kufanya vizuri zaidi.