Connect with us

Makala

Dilunga Kupigwa Kisu

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba sc Hassan Dilunga yupo mbioni kufanyiwa upasuaji wa goti baada ya kuumia na huenda akakosa michezo yote ya klabu ya Simba sc iliyobakia msimu huu.

Dilunga mwenye uwezo wa kucheza nafasi zote za kiungo amekosekana uwanjani kwa muda mrefu kutokana na majeraha hayo na tayari uongozi wa klabu ya Simba sc unampango wa kumfanyia upasuaji.

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema Dilunga bado anaendelea na matibabu pengine msimu huu hatashiriki kuukamilisha kutokana na majeraha yanayomsumbua
“Ni kweli, Dilunga bado ni mgonjwa na pengine anaweza asionekane kabisa katika mechi zilizobaki msimu huu kutokana na kuumia goti na uongozi unafanya utaratibu wa kumfanyia upasuaji,” alisema Ahmed.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala