Connect with us

Makala

Coastal,Singida Big Stars Hakuna Mbabe

Mchezo wa ligi kuu nchini kati ya Singida Big Stars na Coastal Union ya mkoani Tanga umemalizika katika uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga bila mbabe baada ya kutoka sare ya 1-1 baina ya timu hizo.

Greyson Gerrad alianza kuipatia Coastal Union bao la mapema dakika ya 44 na kipindi cha pili Bright Adjei alipambana na kuisawazishia Singida Big Stars dakika ya 74 ya mchezo na kufanya mpaka filimbi ya mwisho inamalizika kwa sare ya 1-1.

Kutokana na matokeo hayo sasa Coastal Union wanakua katika nafasi ya 13 ya msimamo wa ligi kuu wakiwa na alama 26 huku Singida Big Stars wakiwa katika nafasi ya tatu na alama 49 huku timu hizo zikiwa zimecheza michezo 25 ya ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala