Connect with us

Makala

Chelsea Wapigwa Fainali FA

Klabu ya Chelsea imelikosa kombe la Fa baada ya kufungwa kwa penati na Liverpool Fc katika mchezo wa fainali uliofanyika katika dimba la Wembley nchini Uingereza.

Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika timu hizo zilikua suluhu pamoja na dakika 30 za nyongeza pia hakuna timu iliyopata goli hali iliyomlazimu mwamuzi kuamuru mapigo ya penati ambapo Liverpool walishinda kwa penati 6-5 za Chelsea huku ikiwa zimepita siku 76 tu tangu Chelsea wafungwe katika michuano ya kombe la Carabao na kupelekea nafasi kwa Liverpool kuchukua makombe manne msimu huu.

Eduard Mendy alifanikiwa kumzuia Sadio Mane asiipe ushindi Liverpool baada ya kupangua penati yake lakini umakini wa Kipa Allison Becker aliyecheza penati ya Mason Mount iliyowarudisha mchezoni Liverpool na Kostas Tsimikas alifunga penati ya ushindi kwa Liverpool na kufikisha makombe mawili msimu huu ambayo yote wameyapata kwa kumfunga Chelsea fainali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala