Connect with us

Makala

Chama Mbioni Kurejea Simba sc

Kiungo Cletous Chama ameanza kukamilisha taratibu za kuvunja mkataba wake na klabu ya Rs Berkane ya nchini Morroco ili kurejea nchini kujiunga na klabu yake ya zamani ya Simba s.

Chama alisajiliwa na Berkane kwa mkataba wa miaka mitatu kwa dau linalokadiriwa kufikia milioni mia nane huku yeye akivuta pesa ndefu ya usajili lakini kukosa furaha na maisha ya Morroco imekua ni sababu ya kiungo huyo kuomba kurejea nchini kujiunga na klabu yake ya zamani huku Yanga sc nayo ikimhitaji.

Simba sc wako tayari kumpokea staa huyo lakini kwa sharti la kutovunja mkataba wake hivyo suala hilo akilifanya mchezaji mwenyewe ili awe huru kurejea sehemu ambaye aliishi kifalme na moyo wake ulipo.

Kiungo huyo baada ya kutamba nchini kwa misimu kadhaa alishinikiza kuuzwa kwenda RS Berkane inayonolewa na kocha Frolent Ibenge lakini hali tofauti ya kimazingira imemfanya akose furaha klabu hapo huku akiwa hajapata nafasi ya kuonyesha uwezo wake.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala