Connect with us

Makala

Chama Abaki Dar

Licha ya msafara wa pili wa klabu ya Simba sc kuondoka kuelekea kambini nchini Uturuki bado staa wa timu hiyo Cletous Chama amebaki jijini Dar es salaam ikitaarifiwa kuwa kuna mambo ya kiofisi anashughulikia.

Msafara huo wa pili unajumuisha mastaa wapya kama Fabrice Ngoma,Che Fondoh Malone,Aubin Kramo,Jean Baleke na wengine ambao walibaki hapa nchini kukamilisha baadha ya taratibu za usajili na safari.

“Kundi la pili limeondoka alfajiri ya leo na Chama hajaondoka kwenda Uturuki, suala lake lipo katika uongozi wa juu wakijaribu kulishughulikia litakapoamriwa basi tutawajulisha.” Meneja wa habari na mawasiliano Simba SC, Ahmedi Ali akizungumza ndani ya Sports Bando ya 107.3 UFM.

Chama inadaiwa ana mgogoro wa kimkataba na uongozi wa klabu hiyo ambapo kuna baadhi ya mahitaji yanapaswa kutimizwa wakati huu hasa dau la usajili ambalo lililipwa nusu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala