Connect with us

Makala

Carlinhos Atua Rasmi Yanga

Fernandes Guimaraes ‘Carlinhos’ tayari ameshatua kwenye ardhi ya Tanzania akitokea Angola kwaajili ya kumalizana na mabosi wa Yanga Sc ili kuanza rasmi kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake Jangwani.

Kiungo huyo alikuwa anakipiga ndani ya Petro de Luanda ya nchini Angola ambapo alifanikiwa kutupia jumla ya mabao tisa na kutoa pasi tano za mabao.

Carlinhos alikubali kusaini dili la miaka miwili ndani ya Yanga Sc hivyo leo amekuja kukamilisha dili hilo ili kuanza mazoezi rasmi na wanajangwani hao ambao walishaanza maandalizi ya kuelekea wiki ya wananchi siku Jumapili Agosti,30.

Yanga Sc ina malengo ya kuwatambulisha nyota wake wapya na wale ambao walikuwa na kikosi msimu uliopita katika siku hiyo ya Yanga Day ambapo pia inasadikika mwanamziki wa kizazi kipya,Harmonize ‘Konde Boy’atakuwepo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala