Connect with us

Makala

Cameroon Wafuzu Kimiujiza

Timu ya Taifa ya Cameroon imefanikiwa kufuzu kombe la Dunia nchini Qatar mwakani baada ya kufanikiwa kuifunga Algeria mabao 2-1 ugenini katika uwanja wa Mustapha Tchaker.

Cameroon iliingia mchezoni ikiwa imefungwa mchezo wa awali nyumbani kwa bao 1 huku kocha Rigobert Song akiwa na shinikizo la matokeo chanya kutoka kwa swahiba wake Samuel Etoo ambaye ni rais wa shirikisho la soka nchini humo.

Erick Choupo Moting alifunga bao la kusawazisha dakika ya 22 lakini furaha ya Simba wasiofungika ilizimwa dakika za nyongeza 30 baada ya dakika 90 kumalizika kwa pande zote zikiwa sawa 1-1 ambapo dakika ya 118 Algeria walipata bao la kusawazisha katika mchezo huo na lililowafanya waongoze 2-1 katika matokeo ya jumla lakini fiuraha yao ilizimwa dakika tatu kabla ya mchezo kuisha baada ya Cameroon kupata bao la pili kupitia kwa Karl Toko Ekambi dakika za nyongeza za mwisho mwa mchezo.

Cameroon wanafuzu kwa matokeo ya jumla ya 2-2 ambapo wanabebwa na bao la ugenini baada ya kufunga mabao mawili ugenini na kuungana na Ghana,Senegal,Morroco na Tunisia kuwakilisha bara la Afrika katika michuano ya kombe la dunia huku vigogo kama Nigeria,Misri pamoja na Ivory Coast wakishindwa kufuzu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala