Connect with us

Makala

Caf Yaipa Mzuka Simba sc

Simba wamepata mzuka wa aina yake baada ya CAF kuruhusu kuingiza mashabiki zaidi ya nusu kwenye Uwanja wa Mkapa Jumapili dhidi ya Berkane katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Habari za ndani kutoka Simba sc zinadai kwamba uongozi wa klabu hiyo waliomba Shikirikisho la Soka Afrika (Caf) waingize mashabiki 60,000 ili kujaza uwanja katika mchezo wa wikiendi dhidi ya Berkane ya Morocco.

Hata hivyo, Caf imewapa mashabiki 35,000 ambao ni zaidi ya nusu ya uwanja huo unaobeba mashabiki 60,000 hivyo kuwapa ahueni kutokana na umuhimu wa mashabiki viwanjani huku Simba sc ikihitaji kushinda ili kujiwekea mazingira sawa ya kufuzu kutokana na kupoteza mchezo wa awali kwa Berkane kwa kipigo cha mabao 2-0.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala