Connect with us

Makala

Beki Azam Fc Aitwa Senegal

Beki wa klabu ya Azam fc  Cheikh Tidiane Sidibe amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Senegali ‘Simba wa Teranga’ kwaajili ya maandalizi ya mchezo mmoja wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 dhidi ya Rwanda utakaochezwa Septemba 9 mwaka huu.

Sidibe amekua mchezaji pekee anaecheza ligi kuu Tanzania Bara kujumuishwa kwenye kikosi cha Simba wa Teranga ambao  wamewaacha nyota wao wengi wa kikosi cha kwanza.

Hata hivyo tayari Senegali wamekwisha fuzu kwenda AFCON kwakuwa tayari wanaongoza kundi L wakiwa na pointi 13 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yeyote katika kundi hilo na nafasi ya pili inashikwa na Msumbiji na pointi 7, Benin pointi 5 na Rwanda pointi 2.

Sidibe amesajiliwa na Azam Fc msimu huu ambapo mpaka sasa amecheza katika michezo yote ya ligi kuu na ya kimataifa akiwa na klabu hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala