Connect with us

Makala

Barcelona Waanza Mazoezi

Mabingwa wa La Liga,Barcelona siku ya jana walirejea kwenye uwanja wao wa mazoezi uliopo katika mji mkuu wa Catalan wakiwemo Lionel Messi ,Luis suarez na wachezaji wengine wa Barca.

Barca walikuwa wakiendesha mazoezi kwa wachezaji binafsi huku kikosi kikigawanywa katika sehemu tatu uwanjani wakitekeleza agizo la kutokaribiana baada ya kikosi kupimwa na kufanyiwa taratibu zote za afya.

Wachezaji hao waliambiwa kuwasili moja kwa moja uwanjani wakiwa na vifaa vyao vya mazoezi ,na kurudi mara moja nyumbani baada ya kumaliza mazoezi yao bila ya kuingia katika vyumba vya kubadilishia nguo.

Walifanya mazoezi kwa muda tofauti na wameendelea leo Jumamosi pia walipost picha zao wakifanya mazoezi kwa mara ya kwanza tangu kusimamishwa kwa shughuli zote za michezo kutokana na virusi vya Corona.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala