Connect with us

Makala

Barca yaweka Paundi Bilioni 1 kumuuza Pedri

Ni sawa na kusema kuwa Barcelona hawana kabisa na wala hawawazi kumuuza kinda wao Pedri kwa kuweka kipengele cha kumuuza(release clause) chenye thamani ya Paundi Bilioni moja za Kiingereza kwa klabu itakayotaka kupata saini ya kiungo huyo siku za usoni.

Kiungo huyo mwenye miaka 19 zao la akademi ya soka ya klabu hiyo La Masia amekuwa kwenye kiwango bora na kuwashangaza wapenzi wa soka duniani tangu alipopandishwa kikosi cha wakubwa msimu uliopita na kocha mkuu Ronald Koeman.

Pedri aliitwa na kuichezea timu ya Taifa ya Hispania katika michuano ya Euro 2020 ambapo alicheza mechi zote hadi hatua ya nusu fainali walipotolewa na Italia kwa mikwaju ya penati,baada ya michuano hiyo aliitwa tena kwenye kikosi cha Hispania kilichoshiriki michuano ya Olimpiki nchini Japan walipofungwa fainali na Brazil.

Barcelona wameweka kipengele hicho baada ya Pedri kusaini mkataba mpya wa miaka mitano wakimuona kama almasi na taswira ya timu hapo baadae hivyo hawataki kumpoteza.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala