Connect with us

Makala

Banka Awasubiri Mtibwa

Wakati akitarajiwa kuibeba tena timu yake itakaposhuka dimbani dhidi ya Mtibwa Sugar leo, kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mohamed Issa ‘Banka’, ametoa siri ya kuendelea kucheka na nyavu

Banka amefunga mfululizo wakati huu akitokea chumba cha majeruhi, ambapo kabla ya juzi kutupia dhidi ya Jamhuri kwenye mechi ya Kombe la Mapinduzi, pia alifunga dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Katika mechi hiyo ya juzi iliyopigwa Uwanja wa Amaan na Yanga kushinda 2-0, Banka alitokea benchi kipindi cha pili na kutupia dakika ya 85 baada ya Adeyum Saleh kutangulia kuziona nyavu dakika ya 45.

Kiungo huyo fundi amewataka mashabiki wa Yanga kufurahia matunda yake baada ya kumvumilia kipindi akiwa majeruhi.

“Siri kubwa ya mafanikio haya ni mazoezi na kujituma, lakini pia ushirikiano mkubwa ninaopata kutoka kwa wachezaji wenzangu

“Nawaomba mashabiki wa Yanga waendelee kutuunga mkono watafurahia ubora wetu katika mechi zinazofuata,” Banka alisema.

Akiuzungumzia mchezo wa nusu fainali leo dhidi ya Mtibwa Sugar, Banka amesema utakuwa mgumu kwa kuwa ni timu inayowafahamu vizuri.

“Mtibwa tunacheza nao ligi moja na ni timu bora, hautakuwa mchezo mwepesi, lakini tumekuja kupambana,” alisema.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala