Connect with us

Makala

Bangala Atua Azam Fc

Klabu ya Yanga sc imefikia makubaliano na klabu ya Azam Fc juu ya kumnunua kiraka Yannick Bangala kwa dau la kiasi cha shilingi milioni 100 ambapo tayari klabu hiyo imethibitisha kuhusu dili hilo kukamilika.

Bangala alisaliwa na mkataba wa mwaka mmoja klabuni hapo ambapo tayari alishaonesha nia ya kutaka kuondoka Yanga sc ambapo klabu ilikua tayari kumuachia kwa sharti la kutojiunga na klabu yeyote kutoka Tanzania.

Baada ya vuta nikuvute ya muda mrefu hatimaye makubaliano yamefikiwa kwa pande mbili kuachana baada ya Azam Fc kuwasilisha ofa ya dau la shilingi milioni 100 na kufanikiwa kumsajili staa huyo.

Bangala amekaa Yanga sc kwa misimu miwili na amefanikiwa kuchukua makombe yote ya ndani hivyo kupata changamoto mpya ndani ya klabu nyingine hapa nchini ni jambo jema kwake.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala