Connect with us

Makala

Bangala Arejea Azam Fc

Baada ya kuwa nje ya dimba kwa muda wa wiki moja akiuguza majeraha ya misuli ya paja nyota wa klabu ya Azam Fc  Yannick Bangala amerejea rasmi kwenye mazoezi ya kawaida na wachezaji wenzake kujiandaa na mechi zijazo.
Bangala amerejea wakati kikosi cha klabu hiyo kikifanya mazoezi ya mwisho na tayari leo mapema  Ijumaa Alfajiri ameungana katika  safari ya kuelekea Ethiopia kukipiga na Bahir Dar Kenema.
Azam Fc inakabiliwa na mchezo wa awali wa kombe la shirikisho la Caf dhidi ya klabu hiyo ambao utafanyika nchini Ethiopia ambapo kama atafuzu ataingia hatua ya pili na akifuzu moja kwa moja watakata tiketi ya kuingia hatua ya makundi.
Bangala amejiunga na Azam Fc msimu huu baada ya kuuzwa na Yanga sc kwa dau la kiasi cha shilingi milioni 100 lakini alipata majeraha siku chache tu baada ya kujiunga na klabu hiyo hali iliyomfanya akose michuano ya ngao ya jamii.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala