Connect with us

Makala

Banda Akubali Yaishe

Winga Peter Banda amekubali kuondoka katika klabu ya Simba sc baada ya kupata ofa sehemu nyingine na kumaliza mgogoro wake na klabu hiyo ambayo ilikua na nia ya kumtoa kwa mkopo.

Inasemekana kuwa Banda aligomea kutolewa kwa mkopo akitaka aachwe moja kwa moja akatafute malisho sehemu nyingine lakini kuwasili kwa ofa hiyo kumelifanya jambo hilo kuwa rahisi kwa pande zote mbili.

Kuondoka kwa Banda kutarahisisha usajili wa Luis ambapo Simba sc inapambana kukamilisha dili la winga huyo pamoja na kipa mpya huku tayari kikosi ilikuwa na nyota 12 wa kigeni kwa mujibu wa sheria ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lakini kuibuka kwa ofa ya Banda  imewapa nguvu Simba sc kumalizana na Al Ahly ili kumrejesha Luis huku pia ikidaiwa kuwa Sakho nae tayari amepata timu hivyo anaweza kuondoka.

Usajili wa kipa na Luis unasubiriwa kwa hamu na wanasimba wengi huku wakiwa na mioyo safi kuwaruhusu Banda na Sakho kuondoka kutokana na orodha ya majembe waliyosajili.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala