Connect with us

Makala

Baleke Hatari Tupu

Mshambuliaji wa klabu ya Simba sc Jean Baleke amedhihirisha umahiri wake katika kuzifumania nyavu baada ya kufunga mabao matatu katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu nchini uliofanyika katika uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.

Iliwachukua Simba sc dakika 3 pekee kupata bao la uongozi likifungwa na Baleke baada ya kumzidi maarifa beki wa Mtibwa Sugar huku pia akifungwa mengine dakika za 7 na 34 kwa nzuri ya viungo washambuliaji wa klabu hiyo wakiongozwa na Saido Ntbanzokiza na Cletous Chama.

Simba sc sasa imefikisha jumla ya alama 57 katika michezo 24 ya ligi kuu nchini huku ikiwa katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi hiyo na ikikabiliwa na kibarua kigumu cha kuvaana na Ihefu Fc mchezo unaofuata wa ligi kuu ugenini mkoani Mbeya.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala