Mshambuliaji wa klabu ya Simba sc Jean Baleke amepeleka kilio katika klabu ya Coastal union baada ya kufunga mabao matatu katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa uhuru ambapo klabu yake ya Simba sc iliibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Coastal Union inayonolewa na kocha Mwinyi Zahera ilionekana kuupania mchezo huo lakini kukosa umakini kwa timu nzima hasa mabeki kuliwafanya kufanya makosa ya kizembe yaliyopelekea kufunga mabao ya haraka haraka.
Bao la kwanza uzembe wa walinzi kumkaba Cletous Chama ambaye alimpasi Baleke aliyefunga bila bugudha yeyote dakika ya saba ya mchezo huku dakika nne baadae akafunga tena kiulaini akimalizia pasi kutoka kushoto mwa uwanja.
Jose Luis Miqquisone aliangushwa katika eneo la hatari ambapo mwamuzi Ahmed Arajiga aliamuru ipigwe penati na Baleke alifunga tuta hilo dakika ya 38 ya mchezo na kufanya timu kwenda mapumziko matokeo yakiwa 3-0.
Kipindi cha pili hakikua na maajabu yeyote kwa timu zote mbili zaidi ya kosakosa za magoli ambapo mpaka dakika 90 za mchezo matokeo yalibaki kuwa 3-0.
Simba sc sasa imesogea katika nafasi ya pili ya msimamo ikiwa na alama 9 na wastani wa magoli 7 huku Azam Fc ikiwa katika nafasi ya tatu ikiwa na alama sawa na Simba sc huku Yanga sc nao wakiwa na alama sawa na Simba sc japo wana wastani wa mabao 11.