Connect with us

Makala

Aziz Ki Atwaa Tuzo April

Mchezaji wa klabu ya Yanga sc Stephane Aziz Ki ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu nchini kwa mwezi April akiwashinda Jean Baleke na Ayoub Lyanga wa Azam Fc ambao aliingia nao katika fainali.

Aziz Ki ameteuliwa na kamati maalumu ambayo hufanya tathmini ya viwango vya wachezaji iliyoko katika bodi ya ligi kuu nchini ambapo kwa mwezi wa nne staa huyo amefunga mabao matatu katika mchezo mmoja dhidi ya Kagera Sugar ambao timu hiyo iliibuka na ushindi wa mabao 5-0.

mbali na Aziz Ki pia kamati hiyo imemchagua kocha Abdalah Mohamed wa klabu ya Tanzania Prisons kuwa kocha bora wa mwezi akiwashinda Roberto Oliveira wa Simba sc na Daniel Cadena wa Azam Fc huku meneja wa uwanja wa Highlanders Estates uliopo Mbarali unaomilikiwa na klabu ya Ihefu Omary Malule kuwa meneja bora wa uwanja akichukua tuzo hiyo kwa mara ya nne mfululizo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala