Connect with us

Makala

Azam,Biashara zasonga mbele CAF

Wawakilishi wa Tanzania katika mashidano ya kombe la shirikisho barani Afrika Azam FC na Biashara United zimefanikiwa kufuzu hatua ya awali ya michuano hiyo baada ya kuinuka na ushindi hii leo.

Azam wamepata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Horseed ya Somalia na kufanya matokeo ya jumla baada ya michezo miwili kuwa 4-1,goli pekee la mchezo lilifungwa na  Kader dakika ya 39 kipindi cha kwanza na kuwawezesha matajirim hao wa jiji la Dar es salaam.

Azam Fc watakutana na Pyramids FC ya Misri katika mchezo wa kufuzu kuingia makundi ya kombe la shirikishi kwa vilabu.

Wanajeshi wa mpakani Biashara United wao wameibuka na ushindi wa 2- dhidi ya Dikhil ya Djibou katika mchezo uliofanyika katika dimba la Chamazi,magoli yote mawili yamefungwa na kiungo mkongwe Ramadhan Chombo ‘Redondo katika kipindi cha kwanza na kuwapa Biashara ushindi wa jumla wa 3-0 baada ya ushindi wa ugenini wa 1-0.

Wawakilishi wengine wa Tanzania katika michuano ya kimataifa Wananchi Yanga kesho watakuwa kibaruani nchini Nigeria dhidi ya wenyeji Rivers United ambao walishinda 1-0 Dar es salaam.Yanga wana kazi kubwa ya kupindua matokeo ugenini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala