Connect with us

Makala

Azam Fc Yashusha Mtambo wa Mabao

Klabu ya soka ya Azam Fc imekamilisha usajili wa mshambuliaji hatari Alassane Diao akitokea US Goree ya nchini Senegali ambapo amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili mpaka msimu wa 2026 akichukua nafasi ya Rogers Kola ambaye ametemwa.

Usajili huu ni moja kati ya sajili nne ambazo Azam Fc wamepanga kuzifanya huku wakiwa tayari wamewasajili Feisal Salum na Gibril Sillah huku wakisubiri kumtambulisha staa mwingine ambaye ni beki.

“Tunayo furaha kuwataarifu kuwa tumeingia mkataba wa miaka miwili na mshambuliaji hatari kutoka Senegal, Alassane Diao, akitokea US Goree”ilisomeka taarifa kutoka Azam Fc.

Us Goree ni moja ya timu ya daraja la kati inayoshiriki ligi kuu nchini Senegal ambapo katika msimu wa ligi kuu 2022/2023 ilimaliza katika nafasi ya nane.

Azam Fc msimu ujao imedhamiria kufanya vizuri ambapo msimu huu umemalizika ikiwa katika nafasi ya tatu ya msimamo na kufanikiwa kupata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa katika kombe la shirikisho ambapo pia Tanzania kama nchi imepata nafasi nne za klabu kushiriki huku Simba sc na Yanga sc wakishiriki michuano ya kombe la klabu bingwa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala