Connect with us

Makala

Azam Fc Yapiga 4-1 na Wydad

Klabu ya Azam Fc imekubali kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Wydad Casablanca inayonolewa na kocha Rulani Mokwena katika mchezo uliofanyika katika uwanja uliopo katika mji wa Benslimane nchini Morocco ikiwa ni mchezo wa mwisho kwa klabu hiyo kabla ya kupita Rwanda kisha kurejea nchini.

Azam Fc baada ya kipigo hicho sasa itakwenda nchini Rwanda kucheza na Rayon Sports katika mchezo maalumu wa kuadhimisha siku ya “Rayon Day” jijini Kigali huku pia ikitumia fursa hiyo kutambulisha wachezaji wake wapya nchini humo ikilenga zaidi kujitangaza na kuvuna mashabiki.

Cheikh Sidibe alifunga goli la kwanza dhidi ya Azam Fc kwa penati dakika ya 39 lakini bao hilo lilisawazishwa na Mohamed Rayhi kabla ya mapumziko huku kipindi cha pili mvua ya mabao ikiishukia Azam Fc ambapo wachezaji Mounir El Habach, Chouaib Faidi and Mohamed El Ouardi walifunga mabao na kukamilisha idadi ya  4-1.

Azam Fc ikirejea nchini itakua na kibarua kizito cha kukutana na Coastal Union katika mchezo wa ngao ya jamii utakaofanyika Augusti 8 katika uwanja wa Amani Visiwani Zanzibar.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala