Klabu ya Azam Fc imefanikiwa kupata alama moja katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba sc baada ya kufanikiwa kuvuna alama moja katika mchezo hup uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.
Ikianza na washambuliaji wenye kasi wakiongozwa na Prince Dube pamoja na Abdul Sopu Azam Fc ilifanikiwa kupata bao la mapema sekundi ya 17 ya mchezo likifungwa na Dube aliyepokea pasi safi ya James Akaminko na kufanikiwa kumchambua kipa Aishi Manula.
Simba sc iliyoanza na John Boko eneo la mbele akisaidiwa na Chama na Saido Ntibanzonkiza ilikosa nafasi nyingi za wazi kipindi cha kwanza kiasi cha kuufanya mchezo kuwa mgumu zaidi ambapo hata alipoingia mshambuliaji Jean Baleke bado hali ilizidi kuwa ngumu kupata bao la kusawazisha.
Kuingia kwa Kibu Dennis dakika za mwisho mwa mchezo kuliongeza nguvu Simba sc na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika za nyongeza ambapo Kibu Dennis alipiga mpira uliounganishwa na beki wa Azam Fc aliyekua katika harakati za kuokoa na kujifunga.
Baada ya kusawazisha bao hilo Simba sc ilijitahidi kupata bao ka ushindi lakini milango ilikua migumu na kuambulia kugawana alama moja kwa kila timu na kuzidi kufifisha matumaini ya kurudisha ubingwa wa ligi kuu uliopotelea Jagwani msimu uliopita.
Simba sc sasa imefikisha alama 54 nafasi ya pili ya msimamo huku Azam Fc akiwa na nafasi ya tatu na alama 44 na kumuacha Yanga sc kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini.