Connect with us

Makala

Azam Fc Hali Tete

Klabu ya Azam Fc imerejea nchini mikono nyuma baada ya kukubali kufungwa mabao 3-0 na klabu ya Al Akhdar ya nchini Libya katika mchezo wa kombe la shirikisho hatua ya pili mchezo uliofanyika katika uwanja wa Benina Martyrs uliopo kilomita 19 kutoka mji wa Benghazi nchini humo.

Al Akhdar ilianza mchezo kwa kasi na kufanikiwa kupata mabao ya haraka haraka kupitia kwa Suhaib Sulaiman aliyefunga kwa penati dakika ya 11 kisha Edward Manyama alijifunga dakika ya 36 na Amer Mohamed Altaweg kufunga bao la tatu dakika ya 41 na mpaka mapumziko tayari wenyeji walishajihakikishia ushindi kutokana na kuwa na mtaji mkubwa wa magoli.

Kipindi cha pili licha ya Azam Fc kujitahidi kusawazisha lakini mamabo yalikua magumu na hawana budi kujipanga katika mchezo wa marudiano utakaofanyika hapa nchini katika uwanja wa Chamazi siku jumapili ya Oktoba 16 saa moja jioni ambapo wanatakiwa kupata ushindi wa kuanzia mabao 4 na kuendelea huku wakizuia wasifungwe bao lolote katika mchezo huo ili kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala