Connect with us

Makala

Aucho,Saidoo Majanga Yanga sc

Klabu ya Yanga sc itawakosa mastaa wake Khalid Aucho,Saido Ntibanzokiza na Djuma Shabani kutokana na sababu za kiafya ikiwemo majeraha na kuumwa ugonjwa wa maralia kuelekea katika mchezo wa kesho wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold Fc.

Mchezo huo utakaofanyika katika uwanja wa Ccm Kirumba jijini Mwanza umekua gumzo kutokana na baadhi ya sekeseke ikiwemo kulalamika kwa mashabiki wa Geita Gold Fc kuwa wamehujimiwa kutokana na uongozi wa klabu hiyo kuuhamishia mchezo Mwanza mjini kutoka katika uwanja wa Nyankumbu mkoani Geita.

Yanga sc itawakosa mastaa hao muhimu kikosini kutokana na mchango wao siku za karibuni huku Saido na Aucho wakiwa na majeraha na Djuma akisumbuliwa na maralia.

Yanga sc inawabidi washinde mchezo huo ili kujitengenezea mazingira ya ubingwa mapema kwani mpaka sasa wanaongoza kwa tofauti ya alama nane pekee dhidi ya Simba sc anayeshika nafasi ya pili.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala