Connect with us

Makala

Aucho Ajifunga Yanga sc

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kumuongeza mkataba wa miaka miwili kiungo wake Khalid Aucho kuendelea kusalia klabuni hapo baada ya mkataba wa awali kuelekea ukingoni mwishoni mwa msimu huu wa ligi kuu.

Aucho anaendelea kusalia jangwani baada ya kuwa na msimu mzuri tangu awasili klabuni hapo akifanikiwa kutwaa mataji matatu msimu uliopita ikiwemo ngao ya jamii,ligi kuu na kombe la shirikisho huku tayari msimu huu akitwaa taji la ngao ya jamii kwa kumfunga Simba sc na ameisaidia Yanga sc kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Sasa Yanga sc imetuliza presha za mashabiki kuhusu staa huyo huku pia ikiendelea kupambana kuwabakiza baadhi ya mastaa wengine akiwemo Feisal Salum ambaye amewasilisha barua ya kuvunja mkataba na klabu hiyo huku Dickson Job nae mkataba wake ukielekea ukingoni.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala