Connect with us

Makala

Aubameyang Aongeza Mkataba Arsenal

Pierre-Emerick Aubameyang amekubali kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu ndani ya kikosi chake cha Arsenal ambapo mshahara wake unakadiriwa kuwa pauni 250,00 kwa wiki.

Aubameyang alikuwa kwenye mpango wa kuondoka ndani ya kikosi hicho ila kwa sasa ameonyesha nia ya kuendelea kubaki na kukitumikia kikosi hicho kwa ajili ya msimu wa 2020/21.

Kocha mkuu ,Mikel Arteta pamoja na mabosi wa Arsenal wapo katika kufanya mabadiliko ndani ya timu hiyo  ili kuwa bora ndani ya ligi kuu England pamoja na michuano mingine pia wapo kwenye hesabu za kupata saini ya beki wa Lille,Gabriel Maghalhaes ili kuongeza nguvu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala