Connect with us

Makala

Amazulu Yamtaka Pablo wa Simba sc

Klabu ya Amazulu Fc inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika ya Kusini imeonyesha nia ya kumtaka kocha Pablo Franco Martine aliyetemwa na klabu ya Simba sc kutokana na matokeo mabaya.

Amazulu inayoshiriki ligi kuu ya nchini Afrika ya kusini imeonyesha nia ya kumtaka kocha huyo raia wa Hispania ambapo taarifa kupitia mitandao imeonyesha kuwa barua ya ofa ya klabu hiyo kwa kocha huyo ambayo imesambaa katika mitandao ya kijamii.

Hata hivyo uongozi wa klabu hiyo yenye makao makuu nchini Afrika ya kusini umetoa taarifa ya kuwa haina mpango na kocha huyo ”Kwa mashabiki wetu na nchi kwa ujumla tungependa kuwaarifu kuwa barua hii na habari inayomhusu kocha wa Hispania sio ya kweli”ilisema taarifa hiyo kupitia mitandao ya kijamii ya klabu hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala