Connect with us

Makala

Algeria Yatolewa Afcon

Mabingwa watetezi wa kombe la mataifa ya Afrika(Afcon) timu ya taifa ya Algeria wametolewa katika michuano hiyo baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Ivory Coast katika mchezo wa mwisho wa kundi E uliofanyika katika uwanja wa Douala nchini Cameroon.

Mabingwa hao watetezi wa michuano hiyo walishindwa kuhimili mikikimikiki ya Ivory Coast na kuruhusu bao la kwanza lililofunga na Frank Kessie dakika ya 22 huku dakika ya 39 Ibrahim Sangare akiongeza bao la pili na mshambuliaji wa Arsenal Nicolaus Pepe akifunga bao la tatu dakika ya 54huku dakika ya 60 Riyad Mahrez akikosa tuta na kuwafanya Algeria kusubiri hadi dakika ya 73 kupata bao la kwanza kupitia kwa Sofiane Bendebka.

Algeria imeondoshwa katika mashindano hayo baada ya kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa kundi E akiwa na alama moja huku Sierra Leone ikishika mkia na kuwaacha Ivory Coast na Equatorial Guinnea kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala