Connect with us

Makala

Al Ittihad Yawavuta Mzize na Aziz Ki

Klabu ya Yanga sc imefikia makubaliano na klabu ya Al-Ittihad Fc ya nchini Libya kuwasajili mastaa wake Clement Mzize na Stephan Aziz Ki kwa dau linalokadiriwa kufikia kiasi cha bilioni 4 za kitanzania.

Kazi kubwa sasa iliyopo kwa klabu hiyo ni kufikia makubaliano binafsi na wachezaji hao baada ya klabu ya Yanga sc kukubali kuwauza kwa dau hilo kubwa.

Hata hivyo usajili huo utakamilika wakati wa dirisha kubwa la mwezi juni ambapo kwa sasa klabu hiyo inaangalia mbadala wa mastaa hao ili kuweza kuwasajili mwezi juni.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa Mzize yuko tayari kuchukua dau nono kujiunga na Walibya hao huku Azizi Ki akijaribu kuangalia ofa zingine nzuri zaidi kuliko hiyo.

Yanga sc wamekua wakipokea ofa mbalimbali kuhusu mastaa hao ambapo mara kadhaa klabu ya Wydad Ac imekua ikimfuatilia Mzize ambapo kwa sasa imeamua kumsajili Selemani Mwalimu.

Yanga sc inaona ni vyema kufanya biashara hiyo mwishoni mwa msimu huu ili iweze kusajili mbadala wa washambuliaji hao huku ikiangalia uwezekano wa kumsajili Feisal Salum kutoka Azam Fc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala