Connect with us

Makala

Al ahly,Mamelod Hapatoshi Nusu Fainali Caf

Klabu za Al Ahly Fc ya Misri imeungana na klabu ya Mamelod Sundowns kufuzu hatua ya nusu fainali ya kombe la klabu bingwa barani Afrika baada ya timu hizo kupata matokeo mazuri katika michezo yaoya pili ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Mamelod Sundowns yenyewe ilishinda 1-0 katika mchezo wa awali dhidi ya Esperance de Tunis katika mchezo wa awali nyumbani nchini Afrika ya kusini lakini ugenini pia imefanya vizuri baada ya kulazimisha suluhu katika mchezo huo wa ugenini uliokua na kasi kubwa huku mashabiki wakifurika uwanjani.

Shukrani za pekee ziende kwa mshambuliaji Peter Shalulile ambaye alifunga bao katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizo nchini Afrika ya kusini.

Al ahly kwa upande wao walishinda 1-0 katika mchezo wa awali nchini Misri na jana wakiwa ugenini nchini Mauritania dhidi ya wenyeji Al hilal waliweza pia kuibuka na ushindi wa 1-0 baada ya nyota Emmam Ashour kufunga bao muhimu dakika ya 80 ya mchezo huo na kuzima ndoto za kocha Frolent Ibenge kuipatia timu hiyo ubingwa wa Afrika.

Kwa mujibu wa Caf sasa klabu za Al Ahly na Mamelod Sundowns zitakutana katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika ambapo mchezo wa kwanza unatarajiwa kuchezwa April 18 nchini Afrika kusini na marudiano yatachezwa nchini Misri April 25 2025.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala