Connect with us

Makala

Ajibu Anukia KMC

Inaelezwa kuwa kiungo mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu anaweza kutolewa kwa mkopo kwenda ndani ya klabu ya KMC.

Nyota huyo alijiunga na Simba kwa dili la miaka miwili akitokea klabu ya Yanga ila hajawa na nafasi kwenye kikosi cha kwanza kilicho chini ya Sven Vandenbroeck.

Ajibu akiwa Yanga kwa msimu wa 2018/19 ametoa jumla ya pasi 17 na alikuwa kinara ila msimu huu ndani ya Simba ametoa pasi tano huku kinara wa kutoa pasi ndani ya Simba msimu huu ni Clatous Chama ambaye ametoa pasi 10 za mabao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala