Connect with us

Makala

Aguero,Gurdiola Washikana Mashati

Mshambuliaji wa Manchester city Sergio Aguero ameshikana mashati na kocha wake Pep Guardiola katika mechi iliyoisha kwa sare ya mabao mawili dhidi ya Tottenham Hotspurs katika ligi kuu nchini Uingereza.

Muargentina huyo alionekana kukasirishwa baada ya kufanyiwa mabadiliko dakika ya 66 hali iliyopelekea kutoleana maneno makali na kocha wake wakati akipita kuelekea kuketi katika benchi hali iliyomlazimu kocha msaidizi wa timu hiyo Mikel Arteta kuingilia kati kuwatawanya.

Hata hivyo baada ya Gabriel Jesus aliyeingia kuchukua nafasi ya Aguero alifunga goli la tatu na kurejesha furaha za wawili hao walionekana wakikumbatiana kuashiria furaha waliyokuwa nayo kabla ya mwamuzi kupitia teknoljia ya video(VAR) kulikataa goli hilo.

Mabao ya city katika mchezo huo yalifungwa na Aguero na Sterling huku Lucas Moura na Erick Lamela wakifunga kwa upande wa Tottenham.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala