Connect with us

Makala

Adebayor Ayeyuka Simba sc

Sasa ni rasmi kuwa klabu ya Simba sc ina uwezekano mkubwa wa kumkosa staa wa klabu ya Rs Berkane ya nchini Morocco Victorien Adebayor baada ya klabu hiyo kukataa kumtoa kwa mkopo wakitaka kumuuza jumla jumla kwa dau kubwa ambalo Simba sc wameshindwa kulifikia.

Adebayor ameshakubaliana maslahi binafsi na Simba sc alipokuja nchini na timu yake ya taifa ya Niger kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika mwakani (Afcon 2023) dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania(Taifa stars) huku ikisubiriwa Simba sc kumalizana na Berkane.

Ofa ya Simba sc ilikua ni kumchukua staa huyo kwa mkopo wa mwaka mmoja lakini Berkane wamegomea ofa hiyo wakitaka kumuuza staa huyo moja kwa moja ambapo bei yake ni kubwa ukilinganisha na uwezo wa timu za hapa nchini.

Hii si mara ya kwanza kwa Simba sc kumkosa staa huyo kwani hata msimu uliopita wakati akiichezea timu ya Us Gendamarie ilimkosa kutokana na kuzidiwa na uwezo wa kifedha na Berkane licha ya kuwa staa huyo alikua tayari kutua msimbazi lakini dau la Berkane lilikua kubwa zaidi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala