Connect with us

Makala

Matola Akabidhiwa Vijana Simba sc

Klabu ya Simba imemtangaza kocha Selemani Matola kuwa kocha mkuu wa timu za vijana za Simba,kwa maana ya timu za  chini ya umri wa miaka 17 na ile ya chini ya umri wa miaka 20 ili kuvimbua vipaji ambavyo vitatumika na timu kubwa.

Matola katika majukumu yake hayo mapya anaenda kuanza kibarua cha kuiongoza Simba U17 kwenye ligi ya vijana ya Shirikisho la soka nchini (Tff) ambayo inaendelea viwanja vya shirikisho hilo huko Kigamboni Dar es salaam.

Pia sambamba na jukumu hilo pia atahusika kuiongoza timu ya vijana ya U20 kwenye michuano ya ligi kuu yatakayoanza mapema baada ya ligi kuu kumalizika kama ulivyo utaratibu wa hapa nchini.

Kocha huyo atakua na Jopo lake akiwemo meneja Patrick Rweyemamu ambapo wana jukumu la kuhakikisha Simba wanafikia malengo waliyojiwekea kwenye soka la Vijana ambapo waliahidi kuzunguka nchi nzima kuhakikisha wanawapata vijana sahihi na wenye vipaji ambao watajiunga na timu zao kwa faida ya Simba na taifa kwa ujumla.

“Kwanza tupongeze bodi na uongozi kwa kuona hili, kwetu sisi sio jambo geni. Tulishafanya na tulifanikiwa sana. Naamini sasa tutazalisha vitu vizuri zaidi ikiwezekana zaidi ya ile ya mwanzoni. Sitawaangusha wapenzi wa Simba sc tafanya wanachotaka mimi nifanye kwenye Youth Development.”Akisema Selemani Matola ambaye ni nahodha wa zamani wa klabu hiyo.

Mpira hauwezi kuendelea bila kuwa na uwekezaji kwa vijana. Tulishawahi kufanya hii kazi na matunda yake yanajulikana. Kuanzia 2008 hadi 2015 tumetoa wachezaji takribani 250. Hakuna timu za Ligi Kuu hadi madaraja ya chini hayajawahi kukosa wachezaji ambao wamepita kwenye timu ya vijana ya Simba.”

“Tunatafuta wachezaji wenye vipaji, wenye uwezo, tunatengeneza ajira na tunapunguza mchakato wa usajili sababu kutafuta kitu ambacho hujawekeza kina gharama yake pia kuna kizazi kinapotea kwenye mpira hivyo lazima tuandaje kizazi kipya ambacho kitasaidia Simba na Taifa kwa ujumla.”Alisema Mkuu wa Programu za Vijana wa Simba, Patrick Rweyemamu ambaye amegundua vipaji vya Jonas Mkude,Ramadhani Singano na wengine

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala