Connect with us

Makala

Yanga sc Yapaa Viwango Afrika

Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za mpira wa Miguu (IFFHS) limetoa orodha ya viwango bora kwa klabu za soka barani Afrika kwa kipindi cha Mei 1, 2022 hadi Aprili 30, 2023 ambapo timu mbili za Tanzania zimeingia 10 bora.

Katika orodha hiyo inayovuma tangu asubuhi ya le nchini Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara wanashika nafasi ya 9 Afrika na 104 duniani huku Simba ikishika nafasi ya 10 na 105 duniani.

Nafasi ya kwanza Afrika inashikiliwa na Al Ahly ambaye kwenye nafasi ya duniani yupo namba 5 ambapo kwa muda mrefu klabu hiyo imetesa katika medani za vilabu barani Afrika huku ikiwa na uwezo mkubwa kifedha kiasi cha kusajili mpaka mastaa kutoka ligi kuu nchini Uingereza.

Kupanda kwa Yanga sc katika chati hizo kumezua shangwe kwa mashabiki wa klabu hiyo nchini huku utani wa jadi ukizidi baada ya kuwapita Simba sc katika viwango hivyo ambapo mafanikio hayo ya Yanga sc yamechangiwa na kiwango chao kikubwa katika michuano ya kimataifa hasa kombe la shirikisho nchini ambapo sasa wameingia nusu fainali wakisubiri kucheza na Marumo Gallants mchezo wa marudiano.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala