Connect with us

Makala

Caf Yawajia Juu Al Hilal

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeiandikia barua klabu ya Al Hilal SC ya Sudan juu ya kuzuia vurugu zinazohatarisha mazingira ya Michezo ya ligi ya klabu bingwa barani Afrika wanaocheza Nyumbani unaoitwa Al Hilal Stadium uliopo mjini Omdurman jijini Khartoum nchini Sudan.

Hii imekuja kufuatia Klabu ya Ethiopia S.t George ambao walipeleka malalamiko Caf wakilalamikia suala la Mashabiki wa miamba hiyo ya Omdurman kufanya ghasia zilizopitiliza wakati wa mchezo wa mkondo wa pili wa  hatua ya awali ambao ulimalizika kwa klabu hiyo ya nchini Ethiopia kupoteza kwa bao 1-0 na kuyaaga mashindano hayo.

Aidha CAF imeeleza kama kutakua na taharuki na ghasia za namna hiyo katika michezo inayofuata  hasa dhidi ya Yanga sc watapewa adhabu ya kutoruhusiwa kuingiza Mashabiki Uwanjani katika Mechi zijazo za CAF.

Mchezo unaofuata Al Hilal SC watawakaribisha Young Africans SC ya Tanzania katika mchezo wa Marudiano ya Mzunguko wa kwanza wa ligi ya mabingwa baada ya awali kutoka sare ya 1-1 jijini Dar es salaam.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala