Kocha wa Klabu ya Yanga sc Miguel Gamondi tayari amefanikiwa kuimaliza klabu ya El Merrekh ya nchini Sudan ambao atakutana nao katika mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi siku ya Jumamosi Septemba 16 nchini Rwanda.
Gamondi amefanikiwa kuwasoma mastaa wa kikosi hicho baada ya kunasa baadhi ya video ambapo mastaa wa kikosi cha kwanza cha klabu hiyo walikua wakiitumikia timu ya Taifa ya Sudan katika mchezo dhidi ya Drc Congo katika mchezo wa kuwania kufuzu Afcon 2024.
Katika kikosi cha Sudan kilichocheza juzi usiku na Drc Congo na kufungwa mabao 2-0 jijini Kishansa, kilikuwa na wachezaji wanane wa El Merreikh, huku wengine wakiwa wa Al Hilal iliyowahi kuitibulia Yanga kwenye mechi ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.
Kati ya wachezaji hao, saba walianza kwenye mchezo huo ambao Drc Congo Uliwawezesha kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 zitakazofanyika mapema mwakani huko Ivory Coast, huku Kocha Miguel Gamondi akiwafuatilia kupitia kwenye runinga.
Mastaa hao wa Al Merrikh waliocheza dhidi ya Otoho ni pamoja na kipa namba moja Mohamed Mustafa, beki wa kulia Ramadan Agab, beki wa kushoto Bakhit Khamis na beki wa kati Mohamed Karshoum aliyecheza sambamba na beki wa Al Hilal, Mohamed Ahmed.
Wengine ni mshambuliaji Ahmed Mahmoud na Mohamed Shambaly ambaye alitokea benchi na kati ya mastaa hao walioanza kikosi cha kwanza cha Al Merrikh kinachofundishwa na kocha Osama Nabih ni kipa Mustapha, Agab, Kashroum na Shambaly ambao wana uhakika wa kuivaa Yanga Jumamosi jijini Kigali.
Yanga sc inapambana kufika hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika ambapo mara ya mwisho kufika hatua hiyo ilikua mwaka 1998.