Connect with us

Football

Simba sc Waifuata Dynamos

Kikosi cha Simba sc kimeondoka mchana huu kuelekea Ndola Zambia tayari kwa mchezo wa raundi ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos utakaochezwa Jumamosi hii uwanja wa Levy Mwanawasa.

Kikosi hicho kilichoonekana uwanja wa ndege wa mwalimu J.K Nyerere jijini Dar es salaam kimejaa mastaa wa klabu hiyo akiwemo kipa mpya Ayoub Lakred pamoja na mastaa kama Che Fondoh Malone,Leandre Onana,Cletous Chama,Luis Miqquisone,Moses Phiri,Jean Baleke,Mzamiru Yassin na mastaa wengine kama inavyoonekana hapa.

Simba sc watakua na kazi ya kuhakikisha wanapata matokeo mazuri ugenini ili waje kuimaliza kazi vizuri nyumbani na kufanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika ambapo msimu uliopita walitolewa na Wydad Casablanca hatua ya robo fainali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Football