Connect with us

Makala

Mayele Awalaza Geita Gold Fc

Muuaji Fiston Kalala Mayele ameendeleza moto wake wa kuzifumania nyavu baada ya kufunga bao katika ushindi wa bao 1-0 iliopata klabu yake ya Yanga sc dhidi ya klabu ya Geita Gold Sports mchezo uliofanyika katika uwanja wa Ccm Kirumba jijini Mwanza.

Yanga sc ikiwa inawakosa mastaa kama Khalid Aucho,Saido Ntibanzokiza,Jesus Moloko,Yacouba Sogne na Chico Ushindi ilianza mchezo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la mapema kupitia kwa Mayele sekunde  ya 33 akiunganisha mpira wa kichwa ambao walinzi wa Geita Fc walizembea kuokoa na Mayele akafunga likiwa bao lake la 10 kwa msimu huu wa ligi kuu nchini.

Yanga sc ilikutana na upinzani mkali kutoka kwa Geita Gold Fc ambao walifunguka muda wote wa mchezo wakishambulia na kukaba kwa nguvu huku mshambuliaji wao George Mpole akikosa mabao ya wazi kutokana na kukosa utulivu.

Yanga sc sasa imefikisha alama 45 ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu huku ikiwa imecheza jumla ya michezo 17 huku Simba sc wakiwa katika nafasi ya pili ya msimamo wakiwa na alama 34.

Yanga sc sasa itawavaa Kmc siku ya 16 machi mwaka huu huku ikiwa na kumbukumbu ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa awali uliofanyika mkoani Songea.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala