Connect with us

Makala

Manula Kuwakosa Biashara United

Golikipa wa klabu ya Simba sc Aishi Manula anatarajiwa kuwakosa Biashara United katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya timu hiyo utakaofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Kipa huyo aliyeiongoza klabu ya Simba sc kutwaa ubingwa mara nne wa ligi kuu nchini ataukosa mchezo huo kutokana na matatizo ya kifamilia hivyo nafasi yake inatarajiwa kuzibwa na Beno Kakolanya ambaye ni kipa namba mbili wa klabu hiyo ambaye alisajiliwa kutoka klabu ya Yanga sc.

Simba sc itacheza mchezo huo dhidi ya Biashara United huku ikitegemea ushindi ili kupunguza pengo la alama dhidi ya Yanga sc ambayo inaongoza ligi kwa tofauti ya alama 11 huku ikiwa imetangulia mchezo mmoja zaidi kuzidi Simba sc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala