Connect with us

Makala

Bilionea Aitema Chelsea

Mmiliki wa klabu ya Chelsea fc Billionaire wa Urusi Roman Abramovich  ameikabidhi klabu ya Chelsea mikononi mwa bodi ya wadhamini wa klabu hiyo yenye maskani yake jijini  London nchini Uingereza.
 Hii inakuja siku moja baada ya wabunge wa bunge la Wingereza  kumtaka tajiri huyo kuachana na klabu hiyo kutokana na ukaribu wake na Rais wa Russia Vladimir Putina ambaye anapingwa na mataifa ya magharibi kutokana na kuamua kuivamia kijeshi nchini ya Ukraine kutokana na tofauti za kiitikadi baina ya nchi hizo mbili.
“Kuanzia leo ninawapa bodi ya wadhamini wa Chelsea usimamizi na utunzaji wa klabu nikiwa na imani wataisimamia vizuri huku nikiwakabidhi kila kitu kuanzia wachezaji,wafanyakazi na miundo mbinu yote”Alisema tajiri mwenye uraia wa Urusi Roman Abramovic

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala